simu za dharura
Nyumbani Kuhusu Tovuti Machapisho English Badilisha Mandhari Ingia
Ofisi ya Waziri Mkuu

Kuhusu Idara ya Usimamizi wa Maafa

Ofisi ya Waziri Mkuu — Tanzania Bara

Historia

Historia ya Usimamizi wa Maafa Tanzania

Shughuli za usimamizi wa maafa nchini baada ya uhuru mwaka 1961 zilijikita katika kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa maafa kama vile chakula, dawa, mavazi, makazi ya muda, na vifaa vya malazi. Shughuli hizo zilitekelezwa na serikali kwa kushirikiana na taasisi zisizokuwa za kiserikali zikiwemo Chama cha Msalaba Mwekundu na taasisi za kidini. Vilevile, Serikali ilikuwa ikishirikiana na taasisi za kimataifa zikiwemo Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa na Shirika la Oxfam.

Pamoja na Serikali kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali na taasisi za kimataifa lakini katika kipindi hicho hakukuwa na taasisi ya serikali iliyokuwa na jukumu la moja kwa moja la usimamizi wa maafa. Vilevile, hakukuwa na muundo wa kitaasisi, sera, sheria na miongozo ya uratibu wa maafa. Kutokana na kuongezeka kwa matukio na madhara ya maafa nchini Serikali iliandaa mfumo wa kisera na kisheria ili kuimarisha shughuli za uratibu maafa nchini. Kwa kuzingatia hali hiyo Serikali ilitunga Sheria ya Uratibu wa Utoaji wa Misaada ya Maafa Na. 9 ya mwaka 1990. Sheria hii pamoja na mambo mengine ilianzisha Kamati ya Misaada ya Taifa iliyokuwa na mamlaka ya kupokea na kuidhinisha misaada nchini. Vilevile, Sheria hiyo ilianzisha Idara ya Uratibu wa Misaada ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Hata hivyo, Serikali iliendelea kufanya maboresho katika mfumo wa uratibu wa maafa ambapo mwaka 2003 iliandaa Mwongozo wa Taifa wa Operesheni za Menejimenti ya Mafaa ambao uliweka taratibu za operesheni za maafa na kuainisha majukumu ya wadau wa kukabiliana na maafa.

Aidha, mwaka 2004 Serikali ilitunga Sera ya Taifa ya Menejimeti ya Maafa ambayo inatoa mwongozo katika shughuli za usimamizi wa maafa kwa kuzingatia maeneo yote muhimu ya mzingo wa menejimenti ya maafa ambayo ni kuzuia na kupunguza athari za majanga, kujiandaa, kukabiliana na kurejesha hali pamoja na kuimarisha mifumo ya kiutendaji. Vilevile, Sera hii imezingatia masuala ya upatikanaji wa fedha katika kugharamia shughuli za maafa, mifumo ya tahadhari ya mapema, uhifadhi wa mazingira, makundi maalumu, na ushirikiano wa kikanda na kimataifa. Miongozo mbalimbali iliandaliwa kuwezesha utekelezaji wa sera hii ikiwemo mwaka 2015 kutunga Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Sura ya 242 ambayo iliifuta Sheria ya Uratibu wa Utoaji wa Misaada ya Maafa Na. 9 ya mwaka 1990. Aidha, Serikali iliendlea kuboresha mifumo ya usimamizi wa maafa ambapo mwaka 2022 ilitunga Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Sura ya 242 ambayo ilifuta Sheria ya mwaka 2015 na mwaka 2025 Serikali ilifanya mapitio ya Sera ya mwaka 2004 na kuja na Sera ya Usimamizi wa Maafa ya Mwaka 2004 (Toleo la 2025).

Key Milestones
1961 Uhuru — utekelezaji wa msaada wa kibinadamu unaanza
1990 Sheria ya Uratibu wa Utoaji wa Misaada ya Maafa Na. 9 imetungwa; Idara imeanzishwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu
2003 Mwongozo wa Taifa wa Operesheni za Menejimenti ya Maafa umeandaliwa
2004 Sera ya Taifa ya Menejimeti ya Maafa imetungwa
2015 Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Sura ya 242 imetungwa
2022 Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Sura ya 242 iliyopitiwa imetungwa
2025 Sera ya Usimamizi wa Maafa ya Mwaka 2004 (Toleo la 2025) imepitishwa

Makujumu

Wizara kupitia Idara, itafanya yafuatayo:

(a)
Itatayarisha, kuhuisha na kuratibu utekelezaji wa sera, mipango, sheria, kanuni, mikakati na taratibu za utendaji kwenye shughuli zote zinazohusiana na usimamizi wa maafa Tanzania Bara.
(b)
Itaratibu na kusimamia utekelezaji wa afua za usimamizi wa maafa kwa kushirikiana na wizara, sekta na kamati za kitaalam zenye dhamana ya usimamizi wa maafa katika ngazi zote.
(c)
Itaratibu na kutoa mwongozo kuhusu ushirikiano wa kisekta katika usimamizi wa magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama, visumbufu vya mazao, usugu wa madawa dhidi ya vimelea vya magonjwa, usalama wa chakula na lishe, sumu kuvu, usalama na ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi vya magonjwa na magonjwa yasiyoambukiza.
(d)
Itaratibu wizara, idara, wakala, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa na sekta binafsi katika Utekelezaji wa mikakati, mipango na miongozo ya usimamizi wa maafa.
(e)
Kujiandaa na kukabili dharura zinazovuka mipaka ikiwemo magonjwa ya mlipuko ya binadamu na wanyama na visumbufu vya mazao.
(f)
Itaratibu ushirikiano kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kuhusu usimamizi wa masuala ya dharura na magonjwa ya mlipuko yanayovuka mipaka.
(g)
Itaratibu uandaaji na kusimamia utekelezaji wa miongozo ya tathmini ya hatari za maafa katika miradi mikubwa ya maendeleo.
(h)
Itasimamia utendaji wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura na kukiunganisha na vituo vya kisekta.
(i)
Itaweka mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano utakaowaunganisha wadau wa masuala ya maafa, kufuatilia mwenendo wa majanga na hali ya maafa kwa ajili ya kuchukua hatua za kuzuia na kukabiliana na maafa kwa wakati.
(l)
Itaunda mfumo wa tahadhali ya mapema utakaojumuisha sekta zote na kuwa kiungo kati ya asasi mbalimbali zinazotoa huduma ya tahadhari.
(m)
Itakuza na kuendeleza mafunzo, utafiti, uvumbuzi, elimu kwa umma, mazoezi ya vitendo na nadharia, maarifa, mabadiliko ya tabia na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika usimamizi wa maafa.
(n)
Itatafuta, kuhamasisha na kusimamia matumizi ya rasilimali kwa ajili ya shughuli za usimamizi wa maafa na kuweka miongozo ya ugawaji wa misaada ya huduma za kibinadamu.
(u)
Itaratibu na kusimamia tathmini ya haraka na kina ya uharibifu na mahitaji kwa ajili ya urejeshaji hali kutokana na madhara ya maafa.

Muundo wa Shirika

Muundo wa Idara ya Usimamizi wa Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu
Katibu Mkuu
Idara ya Usimamizi wa Maafa
Sehemu za Idara ya Usimamizi wa Maafa
Sehemu ya Uendeshaji na Uratibu
Sehemu ya Utafiti wa Maafa
Sehemu ya Uendeshaji wa Dharura na Mawasiliano
Sehemu ya Afya Moja
Vitengo vya Msaada
Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
Idara ya Mipango na Bajeti
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Kitengo cha Huduma za Kisheria
Kitengo cha Fedha na Hesabu
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano