simu za dharura
Nyumbani Kuhusu Tovuti Machapisho Elimu English Badilisha Mandhari Ingia
Rudi Nyumbani
news

Hatua za Uokaji katika Mgodi wa Kakonko

April 16, 2026
Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Taasisi ya OpenMap Development Tanzania (OMDTZ), kupitia mradi wa Ramani Zetu, Sauti Zetu, imeendesha warsha ya kupitia na kuthibitisha Mipango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa kata za Makurumula, Mabibo, Keko, Ubungo na Tabata jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo imewakutanisha viongozi wa serikali za mitaa, Kamati za Usimamizi wa Maafa za Kata, wataalamu wa usimamizi wa maafa, waratibu wa maafa wa mkoa na wilaya pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa lengo la kuhakikisha mipango hiyo inakidhi mahitaji halisi ya wananchi wanaoishi katika maeneo yenye hatari ya mafuriko.

Akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni za Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Kanali Selestine Masalamado, amesema ubora wa mpango wa maafa hupimwa kwa uwezo wake wa kutekelezeka na kuleta matokeo chanya kwa wananchi. Amesisitiza kuwa mipango hiyo inapaswa kuzingatia mazingira halisi, rasilimali zilizopo pamoja na uwezo wa taasisi husika ili kuhakikisha jamii zinakuwa salama na zenye ustahimilivu zaidi.

Kanali Masalamado amesema mradi wa Ramani Zetu, Sauti Zetu, unaofadhiliwa na Zayed Sustainability Prize kupitia OMDTZ kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, umefika katika wakati muhimu ambapo mabadiliko ya tabianchi yameongeza hatari ya majanga ya asili ikiwemo mafuriko. Ameeleza kuwa Serikali ina matarajio makubwa kuwa mradi huo utachangia kuimarisha mifumo ya usimamizi wa maafa nchini na kuongeza ushiriki wa jamii katika hatua za kujiandaa na kukabiliana na majanga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa OMDTZ, Bw. Innocent Maholi, amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kujenga jamii zenye uwezo wa kukabiliana na maafa kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa, uchoraji wa ramani shirikishi na uwekezaji katika mifumo ya tahadhari ya mapema. Amesema teknolojia na ushiriki wa wananchi ni nyenzo muhimu katika kubaini maeneo hatarishi na kupanga hatua stahiki za kupunguza athari za maafa kabla hayajatokea.